Alfabeti ya Kigiriki
From Wikipedia
|
Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko wa kuandika lugha ya Kigiriki. Herufi zake hutumiwa pia kama alama za kisayansi.
Alfabeti ya Kigiriki ni alfabeti mama ya lugha za Ulaya. Ni asili ya Alfabeti ya Kilatini ambayo ni mwandiko unaotumiwa zaidi duniani kushinda miandiko mingine. Ni pia asili ya alfabeti za Kikyrili na Kikopti. Kuna miandiko mingine ya kihistoria iliyotokana na Kigiriki.
Asili ya mwandiko huo ulikuwa alfabeti ya Kifinisia. Tofauti kubwa ni alama za vokali na baadaye badiliko la wendo wa mwandiko kutoka kushoto kwenda kulia tofauti na Kifinisia iliyoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto jinsi ilivyo hadi sasa katika mwandiko wa Kiarabu na Kiebrania ambazo ni lugha za kisemiti jinsi ilivyokuwa Kifinisia.
Categories: Mbegu | Mwandiko | Ugiriki | Lugha