Kongo (mto)
From Wikipedia
Mto wa Kongo (kati ya 1971 and 1997 uliitwa Zaire) ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile.
Beseni ya Kongo pamoja na tawimito yake ni eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua. Pia kiasi cha maji pamoja na ukubwa wa beseni yake zina nafasiy a pili duniani baada ya Amazonas huku Amerika ya Kusini.
Jina la mto limepatikana kutokana na Ufalme wa Kongo uliokuwa dola kubwa katika Angola ya Kaskazini na Kongo ya Magharibi wakati wa karne 14-17 BK. Jamhuri zote mbili za Kongo zimepata majina yao kutoka kwa mto.
Mto wa Kongo ni njia muhimu ya mawasiliano na biashara kwa meli zinazoweza kusafiri mle kwa kushirikiana na njia za reli penye maporomoko mahali patatu.
[edit] Tawimito
Tawimito inaorodheshwa kuanzia mdomo kulekea chanzo
- Inkisi
- Nzadi
- Nsele
- Bombo
- Kasai
- Fimi
- Kwango
- Sankuru
- Likuala
- Sangha
- Ubangi
- Giri
- Uele
- Mbomu
[edit] Tazama pia
- Kongo (maana)