Jakaya Kikwete
From Wikipedia
Jakaya Mrisho Kikwete tangu tar. 21 Desemba, 2005 rais wa nne wa Jamhuri ya Maungano ya Tanzania.
Contents |
[edit] Masomo
Amezaliwa 7 Oktoba, 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga. , Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.Lugha ya mama ilikuwa Kikerewe. 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-levels huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mw. 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Daressalaam akimaliza digrii yake mw. 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi
[edit] Familia
Kikwete amezaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Babake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mamake alikuwa mja mzito naye Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake. Jakaya aliposoma Kibaha SS alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Tanga SS alikuwa Head Prefect na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
[edit] Chama na Jeshi
Baada ya kumaliza Chuo Kikuu alijiunga na kazi ya chama cha CCM na Jeshi la Wananchi. Habari zinazopatikana mtandaoni hazikubaliani kuhusu tarehe za vyeo na nafasi mbalimbali alizopewa. Alianza kama Katibu msaidizi wa CCM mashambani. Aliendelea kupanda ngazi kwa kuwa na vyeo mbalimbali katika chama na katika jeshi.
[edit] Kupanda ngazi katika siasa
1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mw. 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa uaraisi upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwal. Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia Benjamin Mkapa nafasi aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri ya Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akishinda uchaguzi wa Disemba 2005 na 80% za kura zote.