Cayenne
From Wikipedia
Cayenne (tamka: kayen) ni mji mkuu wa wilaya na eneo la ng'ambo la Ufaransa la Guyana ya Kifaransa. Kuna wakazi 50,594 (sensa 1999) katika eneo la 23.60 km².
Mji uko kwenye rasi ya nchi kando la mdomo wa mto Río Cayenne unapoishia katika Atlantiki.
Baharini mbele ya pwani kipo Kisiwa cha Sheitani kilichokuwa kisiwa cha gereza cha Ufaransa kati ya 1852 na 1946.