Blogu za mkononi
From Wikipedia
Blogu za mkononi ni aina ya blogu zinazotumia zana zinazoshikika mkononi kama vile simu za mkononi. Kwahiyo, habari, maoni, au visa vinatolewa katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia zana hizi. Teknolojia hii ilianza huko Japan ambapo simu za mkono zenye kamera zilianza kupatikana kwa urahisi.
Inasemekana utumaji wa habari kwenye mtandao wa kompyuta toka katika zana za mkononi ulifanywa na Steven Mann hapo mwaka 1955 alipotumia kompyuta inayovalika. Mwaka 2000 ndipo utumaji wa habari katika mtandao wa kompyuta toka katika simu ya mkono ulifanywa na Tom Paamand nchini Udeni.
Adam Greenfield ndiye aliyeanzisha matumizi ya neno "blogu za mkononi." Aliandaa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Blogu za Mkononi jijini Tokyo, Japani mwaka 2003.