Wolfgang Pauli
From Wikipedia
Wolfgang Pauli (25 Aprili, 1900 – 15 Desemba, 1958) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Austria. Hasa alichunguza nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory) na nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1925 alitangaza Kanuni ya Pauli. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.