Visiwa vya Karibi
From Wikipedia
Visiwa vya Karibi ni idadi ya maelfu visiwa vikubwa na vidogo katika Bahari ya Karibi. Mara nyingi vikundi vitatu vya visiwa hutofautishwa ndivyo:
- Antili Kubwa (Kuba, Jamaika, Hispaniola na Puerto Rico pamoja na visiwa vidogo na funguvisiwa mbalimbali)
- Antili Ndogo (pinde ya visiwa vidogo kati ya Puerto Rico na Venezuela bara kutoka visiwa vya Virgin hadi Antili za Kiholanzi)
- Visiwa vya Bahamas
Vyote vilikuwa koloni za Hispania, Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Denmark au Marekani. Siku hizi vingi vimekuwa nchi za kujitegemea.
Vingine vimekuwa sehemu kamili za nchi zilizopo ng'ambo kwa mfano mikoa ya Ufaransa ya Martinique na Guadeloupe, sehemu za ufalme wa Uholanzi kama Bonaire na Curasao au maeneo ya Uingereza. Vingine vina hali ya katikati; si koloni wala eneo kamili ya nchi ya ya ng'ambo lakini havikutenga na kuwa nchi ya kujitegemea kama Puerto Rico iliyo nchi linaloshiriki na Marekani.
Wakazi mara nyingi ni wa mchanganyiko wa asili ya Kiafrika, asili ya Kizungu na pia ya Waindio asilia pamoja na watu wenye asili ya Asia (hasa Uhindi, Indonesia na Uchina) katika visiwa ambako wafanyakazi walitafutwa ng'ambo baada ya mwisho wa utumwa.
Lugha zinazotumiwa ni hasa Kihispania na Kiingereza pamoja na lugha za Kikreoli. Kufuatana na historia ya ukoloni kuna pia visiwa ambako Kiholanzi (hasa Antili za Kiholanzi) na Kifaransa (Martinique, Guadeloupe, Haiti) hutumiwa.
Orodha inayofuata si kamili.
[edit] Visiwa na funguvisiwa katika Karibi
- Anguilla (Uingereza)
- Antigua na Barbuda
- Antili za Kiholanzi (Uholanzi) pamoja na Bonaire na Curasao
- Aruba (Uholanzi)
- Barbados
- Dominica (Umoja wa Dominica)
- Grenada
- Guadeloupe (mkoa wa ng'ambo wa Ufaransa)
- Hispaniola (pana nchi za Jamhuri ya Dominica na Haiti)
- Jamaika
- Kuba
- Martinique (mkoa wa ng'ambo wa Ufaransa)
- Montserrat (Uingereza)
- Puerto Rico (Marekani)
- Saint Kitts na Nevis
- Saint Lucia
- Saint Vincent na Grenadini
- Trinidad na Tobago
- Visiwa vya Cayman (Uingereza)
- Visiwa vya Virgin vya Marekani
- Visiwa vya Virgin vya Uingereza
Visiwa vya Atlantiki ambavyo mara nyingi huhesabiwa katika Karibi:
- Visiwa vya Bahamas
- Visiwa vya Turks na Caicos