Tewodros II
From Wikipedia
Tewodros II (takriban 1818 – 13 Aprili, 1868) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 11 Februari, 1855 hadi kifo chake. Alimfuata Yohannes III aliyeuzuliwa naye. Jina lake la kubatizwa lilikuwa Kassa Haile Giyorgis. Ingawa hakuwa mrithi wa ufalme aliwashinda wagombea wote vitani. Waingereza walipovamia Uhabeshi chini ya kamanda ya Robert Napier na kushinda jeshi la Uhabeshi, Tewodros II alijiua. Aliyemfuata ni Tekle Giyorgis II.