Shire (mto)
From Wikipedia
Mto wa Shire | |
---|---|
|
|
Chanzo | Ziwa Nyasa (Ziwa Malawi) |
Mdomo | {{{mdomo}}} |
Nchi | Malawi, Msumbiji |
Urefu | 402 km (pamoja na ziwa na tawimto mrefu wa Ruhuhu ina 1200 km) |
Kimo cha chanzo | 474 m (uwiano wa ziwa) |
Mkondo | ?? m³/s |
Eneo la beseni | ?? km² |
Shire ni mto unaotoka katika Ziwa Nyasa (au: ziwa Malawi) ikipeleka maji yake Mto Zambezi.
Kiasi chake cha maji kinategemea kiwango cha maji ziwani. Katika miaka ya 1930 iliwahi kukauka kwa muda; tangu siku zile ilikuwa na maji siku zote.
Shire inatoka kwenye pembe la kusini ya ziwa. Baada ya 10 km inapita katika ziwa la Malombe na kuendelea kwa mwendo wa pole hadi Hifadhi ya wanyama ya Liwonde na Liwonde mjini. Baada ya Liwonde Shire inapita mlimani kwa mtelemko mkubwa zaidi ukipita kwenye maporomoko mbalimbali hasa maporomoko ya Kapichira. Kabla ya kuvuka mpaka wa Msumbiji mto unapita katika tambarare la mabwawa wa Ndinde kusini mwa Malawi kabisa.
Shire inaingia Zambezi takriban 160 km kabla ya mdomo wake baharini.