Pavel Cherenkov
From Wikipedia
Pavel Alekseyevich Cherenkov (28 Julai, 1904 – 6 Januari, 1990) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi. Aligundua mnururisho wa Cherenkov unaotokea elektroni ikitembea kwa mwendo mkali zaidi kuliko mwendo wa nuru. Mwaka wa 1958, pamoja na Igor Tamm na Ilya Frank alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.