Nelly Sachs
From Wikipedia
Nelly Leonie Sachs (10 Desemba, 1891 – 12 Mei, 1970) alikuwa mwandishi na mshairi Myahudi kutoka nchi ya Ujerumani. Mwaka wa 1940 alisaidiwa na rafiki yake Selma Lagerlof kukimbia ukatili wa WaNazi na kuhamia Sweden. Katika mashairi na tamthiliya zake alieleza mateso ya Wayahudi, k.m. katika tamthiliya "Eli: Juu ya Mateso ya Israel" (kwa Kijerumani Eli: Ein Mysterienspiel vom Leiden Israels) iliyotolewa mwaka wa 1951. Mwaka wa 1966, pamoja na Shmuel Yosef Agnon alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.