Talk:Mwanzo
From Wikipedia
Why is the homepage promoting OpenOffice? Just curious.
The user and user talk namespaces should be translated. 66.177.138.113 21:37, 21 Oktoba 2005 (UTC)
---
Contents |
[edit] Makala 200?
Jamani ukurasa ulionyesha makala 199 nikaona niongeze moja tupate 200! Nikatunga "Kaisari" lakini bado 199! Namna gani? --Kipala 00:34, 28 Januari 2006 (UTC)
- Sasa jumla ni 206 (Special:Statistics) au 204 (Mwanzo)! Matt Crypto 14:56, 28 Januari 2006 (UTC)
- Basi tupeane hongera kidogo - bado njia ndefu lakini angalau!! Tuongee tena baada ya kumaliza 250. --Kipala 15:31, 28 Januari 2006 (UTC)
[edit] Kundi: Sayansi + Teknolojia / Makala za Kimsingi
Sioni Falaki. Ninahisi ya kwamba badala yake "unajimu" imeingizwa kwa kuchanganya yote mawili. Falaki ni sayansi ya nyota na anga. Unajimu ni elimu isiyo ya kisanysi ya kutabiri wakati ujao (au: kudai ya kwamba mnajimu ana uwezo wa kutabiri hivyo). Kamusi kadhaa hazieleweki sana katika swali hili au zinachanganya zote mbili vilevile. --Kipala 18:38, 28 Januari 2006 (UTC)
- Basi, sasa nimebadilisha "unajimu" uwe "falaki" katika ukarasa wa mwanzo. Bado watu wanaweza kuandika kuhusu unajimu, lakini wataje kwamba si sayansi. Marcos 12:28, 30 Januari 2006 (UTC)
[edit] Kiswahili cha Microsoft
Wapendwa kampuni ya Bwana Billy yaani "Kalaini-kadogo" wamejitahidi kutoa MS-Windows pia Word kwa Kiswahili. Mimi mwenyewe sijawahi kuiona lakini nimekuta ukurasa ufuatao:
Microsoft Community Glossary for Kiswahili (unajiandikisha kwa jina lolote, anwani barua pepe, neno la siri utakavyo) http://members.microsoft.com/wincg/home.aspx?langid=1089
Wametunga orodha ya maneno yanayohusu mambo ya kompyuta n.k. waliohitaji kutafsiri menyu. Orodha hii ina maneno mengi kushinda kila orodha niliyowahi kuona (kwa mfano http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/sw_TZ_glossary_klnX_1.html), tena maneno tofauti. Kwa mfano: si tena "kompyuta" au "tarakilishi" lakini: "ngamizi".
Kwa mawazo yangu maneno mengi mapya ya Kiswahili yamewahi kutungwa ambayo hayakujali kweli. Yasipotumika basi! Husahauliwa, maneno mapya tena. Lakini kama "Windo" hii inatumika heri tuzoee! Naomba wenzangu watazame ukurasa tupeane mawazo! --Kipala 20:38, 15 May 2006 (UTC)
- Kwa kweli ni mbaya kwamba wanatumia maneno mapya kama "ngamizi". Ninatumaini kwamba watabadilisha neno hilo tena. Lakini sikupata maneno mapya mengine. Maneno mengine ni ya kawaida tu. Je, wewe umepata maneno mapya mengine katika orodha hiyo? Marcos 10:37, 16 May 2006 (UTC)
-
- Ninajua orodha mbili ya maneno ya kompyuta:
- * http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/sw_TZ_glossary_klnX_1.html ni ya The Open Swahili Localization Project (Linux na Open Office) ina maneno kama 700, walikuwa kazini ya kumaliza orodha ya maneno 1500 (sijui wamefika wapi)
- * http://members.microsoft.com/wincg/home.aspx?langid=1089 ni ile ya Microsoft, ina maneno karibu 3000. Ninaelewa kazi imemalizika mwaka 2004, kwa hiyo kompyuta ya microsoft itabaki ngamizi (yangu inaitwa ki-Linux "kompyuta" hata nikiwa na Windows!).
- * sijafanya utafiti kubwa sana lakini naona tofauti. Hapa ni wazo langu tusijali sana yale tunayopendelea lakini tufuate matumizi ya hali halisi. Lakini kwa kikundi kidogo jinsi tulivyo si rahisi hasa kwa sababu wengi wetu wako nje ya Afrika. Je, shule zimeanza kutumia Open Office kwa Kiswahili?? Au ofisi zimeanza kutumia Windows kwa Kiswahili??
- * Mimi naona vema kama wote wetu wanaoandika makala kuhusu habari za kompyuta zinajipatia orodha zote mbili. Halafu tuandike lakini tutumie #REDIRECT ili tuningize maneno ya orodha zote mbili pamoja na yale tunayozoea au kuona katika chat, blogu n.k. kama kawaida.
- * Maarifa kidogo: nimehifadhi (sw-Linux) au nimeakibisha (sw-microsoft) orodha hizi mara mbili katika Excel: nilivyopakua (sw-linux+ms!) zilikuwa katika utaratibu wa ABC ya Kiingereza; halafu nakala ya pili nilipanga katika utaratibu wa ABC-ya Kiswahili. Imenisaidia kutafuta maneno haraka...
- Kwa jumla tusishangae kama kila "kawaida" itabadilika haraka -hivyo ndivyo Kiswahili cha kisasa. --Kipala 19:39, 16 May 2006 (UTC)
[edit] Open Directory Project
If anyone is interested in editing a subcategory in the Kiswahili category: http://dmoz.org/World/Kiswahili/ please apply by clicking on 'become an editor' in the subcategory of choice and following the instructions. :-)
[edit] Maana ya makala hii
Jamani, kuna mwenye kuelewa maana ya makala hii? Nimeisoma nikashindwa kuielewa: http://sw.wikipedia.org/wiki/Semsem_Barabara -- --Ndesanjo
[edit] Tumerudi kwa Kiingereza?
Nimeshangaa kuona kwamba upande wa kushoto tumerudi kwa Kiingereza. Badala ya "Mwanzo" unaweza kubonyeza "Main Page" tu n.k. - bahati mbaya sielewi jinsi ya kurudisha vichwa vya Kiswahili. Naomba virudishwe lakini. Asante! --Oliver Stegen 18:51, 6 Septemba 2006 (UTC)
[edit] Kosa la kuandika neno la "kuhariri"
Kila unapohariri makala yoyote, kichwa chake kinasema "KuhaHiri ..." badala ya "KuhaRiri ...". Naomba irekebishwe. (Samahani, sijui jinsi ya kuirekebisha mimi mwenyewe, ama ningaliifanya.) --Oliver Stegen 21:14, 13 Septemba 2006 (UTC)
[edit] RU
Please add a link to Russian Wikipedia, it contains more than 120 000 articles now! (ru) --82.116.47.194 12:38, 8 Desemba 2006 (UTC)
[edit] Makala maalumu
Nadhani tumefikia kiwango cha makala ya kutosha ili tubadilishebadilishe uso wa ukurasa wetu wa kwanza mara kwa mara. Nimeanza sasa. Wengine wanaojiamini wakiwa na uhakika hawataharibu kitu wachangie pia! Kimsingi ni swali la
- 1 kuteua makala na kubadilisha jina la makala maalumu katika mabano
- 2 kuteua picha nzuri na kuiweka badala ya picha iliyopo (angalia ukubwa! - iliyopo ya Kenya ni 200px)
- 3 kuteua mistari michache ya mwanzo na kuipakia.
--Kipala 17:33, 20 Desemba 2006 (UTC)