Ludwig Quidde
From Wikipedia
Ludwig Quidde (23 Machi, 1858 – 5 Machi, 1941) alikuwa mwanahistoria na mwanasiasa kutoka nchi ya Ujerumani. Alijitahidi kutekeleza amani ya kimataifa, hasa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Mwaka wa 1927, pamoja na Ferdinand-Edouard Buisson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.