Bendera ya Uskoti
From Wikipedia
Bendera ya Uskoti ina rangi ya buluu pamoja msalaba wa Andrea nyeupe. Hii ni msalaba unaolala yenye umbo la "X".
Bendera ya Uskoti ni kati ya bendera za kale kabisa duniani.
[edit] Bendera ya Uskoti kama sehemu ya bendera ya ufalme wa maungano ya Uskoti na Uingereza
Mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa pia mfalme wa Uingereza kwa jina la James I mwaka 1601 akaunganisha bendera za nchi zote mbili kuwa bendera yake ya kifalme. Sheria ya maungano ya Uingereza na Uskoti ya mwaka 1707 ilifanya bendera hii kuwa bendera la kitaifa.
Baadaye bendera ya Eire (Ireland) iliingizwa katika bendera ya maungano ya "Union Jack".
[edit] Hadithi juu ya asili ya msalaba wa Andrea
Waskoti hukumbuka hadithi ya kuwa mfalme aliyeitwa Hungus (au:Angus) aliongoza Wapikti na Waskoti vitani dhidi ya Waanglia na Wasaksoni mnamo mwaka 832 BK lakini akajipata katika hali ngumu pamoja na jeshi lake lote. Alipoombea msaada wa Mungu alimwona Mtume Andrea (aliyesulibiwa kwenye msalaba mwenye umbo la "X") aliyemwahidi ya kwamba atashinda. Asubuhi yake mawingu angani yalipatikana kwa umbo la msalaba wa "X". Waanglia na Wasaksoni walishtuka lakini Waskoti walishika moyo na kushinda.
Tangu zamani ile msalaba wa Andrea umekuwa bendera ya Uskoti.