Barafu
From Wikipedia
Barafu ni maji yaliyoganda. Maji huganda yakishikwa na baridi na kufikia 0°C. Barafu inaeleweka ni maji ya mgando. Hata kiowevu kingine kinaweza kushika baridi na kuganda kuwa barafu ila kama maziwa inaganda tunayaita "barafu ya maziwa".
Inapatikana katika hali na ukubwa mbalimbali. Kama ni ndogo ni fuweli kadhaa tu; kubwa zaidi ni vipande vya mvua mawe. Barafu inaweza kuwa ganda kubwa na nene sana kama lile linalofunika bara ya Antaktika.
Barafu ina kazi muhimu katika hali ya hewa duniani. Hasa maganda ya barafu kwenye ncha za dunia yanatunza sehemu kubwa ya maji matamu yaliyopo.
Maji hupanuka yakiganda. Hivyo barafu yake inahitaji nafasi kubwa kuliko maji ya kiowevo kiasi cha 9%. Mfano wake ni chupa cha soda katika friji kinaweza kupasuka. Sababu yake ni maji ndani ya soda inahitaji nafasi kubwa kuliko soda ya majimaji hivyo kupasua chupa chenyewe.
Kutokana na hali hiyohiyo barafu ni nyepesi kuliko maji hivyo hubaki juu ya maji. Vipande vya barafu vikubwa baharini vinaweza kuharibu hata meli kubwa jinsi ilivyoonyesha mfano wa meli Titanic.
Kwenye mtelemko wa milima barafu yanaweza kutambaa kama mto ikiitwa barafuto.
Makala hiyo kuhusu "Barafu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Barafu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |