Abdus Salam
From Wikipedia
Abdus Salam (29 Januari, 1926 – 21 Novemba, 1996) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Pakistan. Hasa alichunguza usumaku. Mwaka wa 1979, pamoja na Sheldon Glashow na Steven Weinberg alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia, Mwislamu wa kwanza kupata tuzo hiyo.