Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
True Jesus Church - Wikipedia

True Jesus Church

From Wikipedia

True Jesus Church (TJC) ni kanisa ndogo lililoanzishwa Uchina mwaka 1917. Asili yake ni katika mwelekeo wa kipentekoste ndani ya Ukristo.

Inadaiwa ya kwamba TJC lina wakristo milioni 1.5 katika nchi 45. Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hii. Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo mnamo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru". Inasemekana ya kwamba wengi wao ni wa asili ya kichina.

Tangu mwaka 2002 TJC lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nayo tangu 2004.

TJC linashika imani mbalimbali za pekee zinazotofautisha kikundi hiki na makanisa mengine ya kikristo. Kimsingi wanaamini ya kwamba wale wenyewe ni kanisa la kweli la Kristo la pekee; makanisa yote mengine ni ya uwongo. Wanajieleza kwenye tovuti zao ya kwamba Kristo alianzisha kanisa moja la kimitume lililopeleka injili katika nchi mbalimbali. Lakini kanisa hili la mwanzo lilivurugika na imani potovu na uzushi. Katika mwaka 1917 Mungu aliamua kufufua kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na hii ilikuwa mwanzo wa TJC.

Kati ya imani nyingine za pekee ni zifuatazo:

  • atakayebatizwa lazima akubali TJC ni mwili wa Kristo.
  • Wakataza mafundisho ya Utatu wa Mungu wakitumia lugha "Yesu yu Mungu wa kweli".
  • Wanakataza ibada za Jumapili wakidai ya kwamba siku ya Jumamosi ndiyo siku takatifu ya sabato iliyoamriwa kwa Wakristo wote.
  • Hawasheherekei sikukuu za Krismasi na Pasaka kwa sababu wanaamini ya kwamba sherehe hizi zina asili za kipagani na ni mifano ya kuingiliwa kwa imani ya kikristo ya kiasili na uzushi.
  • Wanaangalia desturi ya kuosha miguu kama sakramenti iliyoamriwa na Yesu Kristo.

Mafundisho mengine yanafanana na desturi zinazopatikana hata kati wapentekoste wengine kama vile kusema kwa lugha za roho au ubatizo kwa jina la Yesu kwa kuzamisha chini ya maji tena maji ya kutiririka.

TJC wako kati ya vikundi wanaojitahidi sana kusambaza habari zao kupitia wavuti (intaneti). Tangu 2005 hadi Aprili ya mwaka 2006 wamefaulu kuingiza habari zao katika wikipedia za lugha 114 lakini mara nyingi makala hizo ni tafsiri tu ya maelezo walioandaa wenyewe.

Lugha nyingine
Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com