Ukristo
From Wikipedia
Historia ya Kanisa la Kikristu, Karne za 1-8
DIBAJI Historia ni jambo la pekee, tena jambo gumu lililo na sehemu nyingi.
Awali kuna mambo yatokeayo. Kisha kuna watu wanaotangaza mambo hayo na kushikwa nayo. Nao huandika habari za yaliyotokea kuwaarifu wengine . Jambo gumu lakini, ni kueleza mambo kamili jinsi yalivyotokea. Kama umewahi kuhudhuria barazani , bila shaka umepata kusikia mshtakiwa akisemwa na mashahidi hata wanne wenye ushahidi mbalimbali. Pengine watu hujiona wakisema ukweli, lakini hasira ama wivu ama pendo huwafanya waseme nusu tu ya ukweli.
Kufahamu kamili ukweli wa historia ni kigumu. Ukweli wa historia si kama ule wa hesabu ambao ni hakika isiyobadilika (1+1=2 popote). Tena unapofuata historia ya watu na mawazo yao, ugumu huzidi, kwa kuwa kila mtu, toka mwanzo wake, ni fumbo. Vilevile kila mtu ana kuchukia ama kupendelea kwake bila sababu yenye akili. Kwa mfano, Mfaransa fulani aandikaye historia ya Ufaransa, ataweka ama kukaza mambo mbali na Mwiingereza fulani anayeandika historia hiyo hiyo. Mmoja ataingiza mambo yasiyohesabiwa na mwingine.
Katika biblia yenyewe sehemu fulani ni historia, nyingine ni ngano, ama hadithi. Waandishi wa agano la kale walimsadiki Mungu mmoja hali majirani zao wangali wakisadiki miungu wengi. Wakati wa vita Waisraeli wakadai kwamba Mungu wao alikuwa ameingia kuwasaidia watu wake na kuwadhuru adui zao. Hivyo ndivyo majirani walidai kwamba miungu wao walikuwa wamewasaidia kuwashinda Waisraeli.
Maana watu hao walichanganya ukweli wa historia, ukweli wa ngano na ukweli wa imani.
Sehemu za Agano Jipya vilevile ni historia. Nalo liliandikwa na watu waliompenda Yesu sana na ambao waliamini kwamba alikuwa amefufuka katika wafu na ni Bwana na Mwokozi wa watu wote. Lakini zamani zile palikuwa hapana vitabu vingine vielezavyo habari za Yesu, ila sentensi moja mbili hapo na hapo zinazowasemea watu wanaojiita wafuasi wa mtu filani aliyeitwa Kristu.
Basi kuna aina mbalimbali za ukweli: ukweli wa ngano kama ule wa kitabu cha Mwanzo ama ule wa mababu zetu; ukweli wa historia kama historia ya Tanzania, ama historia ya kanisa letu au dini yetu; kuna ukweli wa hesabu. Pengine aina mbalimbali za ukweli huchanganyika na kama katika biblia. Tena inawezekana ukweli wa aina fulani utabadilika. Ukweli wa hesabu haubadilike, 1akini ukweli wa historia unaweza kubadilika (yaani tunapopata habari zaidi kuhusu jambo fulani, mara kwa mara tunaona kwamba mambo, siyo jinsi yalivyodhaniwa wala kutangazwa mwanzoni). Zaidi ya mambo ya historia yaliyotokea, twapaswa kufahamu maana yake, la hapo, tunatumia mafunzo mengine. Kwa mfano, tunafahamu kwamba Augustini Mt. alidharau ndoa na mambo yahusuyo kiume na kike. Hili ni jambo la historia. Tunajua vilevile kwamba Augustini huyo alikuwa na mwanamke muda wa miaka 16 bila kufunga naye ndoa. Hili ni jambo la historia . Tukitumia mafunzo mengine, kama vile mafunzo ya nia za watu (psychology) tunasaidiwa kufahamu chuki yake Augustini alipodharau ndoa. Kwa mfano, huenda aliona janaa ama hatia kwa sababu ya maisha yake ya zamani. Huu ni mfano kwamba zaidi ya mambo ya historia yenyewe, twapaswa kufahamu maana yake.
Yatubidi pia kuwafahamu waandikao historia, maana nao wana kuchukia na kupendelea kwao bila sababu zenye akili. Ndio kusema pengine watu huandika ili nchi ama kanisa lao litukuzwe ama lisifiwe. Tumewahi kuona hali hio kanisani baada ya Matengenezo ya Kanisa la Uingereza ambapo wanahistoria wakotoliki wamesema uongo juu ya tabia na nia za Waprotestanti. Wanahistoria Waprotestanti vilevile walifanya hivyo hivyo. Ingawaje ni vigumu kuelewa kama habari fulani za historia zina ukweli, lakini hata hapo mafunzo ya historia yana maana sana. Jambo muhimu ni kufahamu kwa nini watu wamefanya hivi badala ya vile, ama kwa nini hali ni hivi, badala ya vile. Kwa mfano, tumejitahidi tangu zamani kufanya mafundisho yote ya dini yawe waziwazi, na kuyaweka katika katekismu. Lakini mambo ya historia yametia mashaka kati yetu. Kwa mfano, huenda tukifundishwa kuwaepuka wapagani ili imani yetu isiharibike. Lakini historia imetutambulisha kwamba Yesu na wafuasi wake hawakufanya hivyo. Bali wakaingia hatarini wakitangaza habari za wokovu ulimwenguni kote.
Mfano mwingine wa hivi karibuni ndio halmashauri za maparokia. Muda wa miaka mingi wengi huwa wamefikiri kwamba ni padre tu anayeweza kukata mashauri yote, na kufanya mambo yote ya kisakramenti. Historia imetusaidia hapo namna gani? Mafunzo ya Agano Jipya na ya kanisa jisi lilivyokuwa mwanzoni wakati wa Mitume hutuhakikishia kwamba mashauri yalikatwa na jumuiya, sio na mtu peke yake. Tena wakati huo, baadhi ya makanisa wakawachagua waliowataka kuwa wenye kutoa masakramenti na kusimamia jumuiya. Halafu mafunzo hayo hutuonyesha kwamba tuna uwezo kurudisha hali ama desturi tuonazo zinafaa. Na mambo mengine yaliyohesabiwa na watu wa zamani kuwa yenye uhakoka kabisa wa historia (kama habari za asili ya wanadamu katika kitabu cha Mwanzo) hufahamika kwamba siku hizi huwa ni ukweli hasa wa ngano kuliko wa historia. Mwishowe, kuna aina mbalimbali za historia. Kuna historia ya watu, ya vita, ya mawazo. Kwa kwe1i historia ya fi1osofia ndiyo historia ya mawazo. Na tunapozungumzia fi1osofia ya kigriki i1iyoingi1ia kanisa, maana yake, ni historia ya mawazo. Vi1evi1e historia ya miundo ya kanisa yaweza kusemeka.
[edit] Muhtasari
Tumeona kwamba historia huandikwa na watu. Na watu mara kwa mara hawawezi kufahamu wala kupasha ukweli kamili. Kwa hiyo ukweli wa historia sio kama ukweli wa hesabu isiyobadilika. Tena kufahamu maana ya historia ni kugumu, kufahamu kwa kiasi kidogo tu hakutusaidii sana. Hata hivyo, lakini, ina maana sana kwetu ikitusaidia kufahamu hali ya mambo jinsi ilivyo sasa. Pia historia ya kanisa inatufahamisha kwamba Mungu hakutuweka hapa duniani na kisha kutusahau wala kutuacha. Bali anaendelea kuingilia kati ya maisha yetu, akitubadilisha na kutufanya watu wapya.
Mtatambua kwamba kitabu hiki ni muhtasari ya historia ya kanisa. Mambo ya historia ni mengi, nasi hatuwezi kuyakuta yote katika dara moja wala kitabu kimoja. Kwa hiyo, kitabu hiki hukaza baadhi ya mambo muhimu katika historia ya kanisa: jinsi kanisa ilivyokuwa zamani kwa zamani; uhusiano kati ya kanisa na serikali; miundo ya kanisa na liturgia yake; baadhi ya mafundisho makuu ambayo yamefumbua imani ya kikristu. Kwani kitabu hiki ni muhtasari hasa, mtabakiwa na maswali mengi.
Kwa kweli kusudi kuu la kitabu hiki ni kuwahimiza mwulize maswali, na kuwakumbusha kwamba sisi wanadamu tunaumba historia yetu , yaani kanisa letu ndilo lile lile tunaloliunda. Tena maneno nayo yasitutiishe. Kweli tuna uwezo na uhuru wa kuiongoza na kuibadilisha miundo ya kanisa lipate kutumikia makusudi yetu tulio wafuasi wa Yesu. Kwa mfano, tukipenda zaidi kudhani kanisa ni Baba ama Mama Mkubwa anayetufariji na kutukomboa, pengine tutajenga majengo makubwa yatakayokuwa ishara za salama na utakatifu. Lakini tukiona kwamba kanisa hasa ni kundi la watu wazima ambao wamejiweka katika kuwatumikia wengine, hatutahanghaikia sana kujenga majengo, bali tutakazana kuimarisha jumuiya za watu walio kanisa. Hapo kanisa sio mahali pa salama, bali ni mtumbwi mdogo, kama ule wa mitume, kwenye mawimbi makubwa baharini. Usalama wetu ni Yesu mwenyewe aliye kati yetu. Kwa hiyo tena twapaswa kujiuliza maswali. Tukiona mambo yamebadilika, tujiulize kama tumefahamu mabadiliko na kama yanafaa. Tujiulize kama mabadiliko hayo huwatumikia watu kweli ama sheria tu. Tujiulize kama yanawatumikia watu wote ama sisi wakristu tu. Tujiulize kama tunathubutu kubadilisha mambo yanayohusu uzima wetu na kama tuko tayari kuwasamehe wanaokosea. Tujiulize kama tuko tayari kushika wajibu wetu wa kuongoza na kuumba historia, ama kama tutaridhika kuongozwa tu.
Mwishowe, mkitumia kitabu hiki darasani, msisitesite kumwuliza mwalimu mengi, tena ukikitumia nyumbani, mwulize padre ama wengine ambao wamewahi kujifunza zaidi historia ya kanisa letu.
NB: Hii ni dibaji tu. Kuna sura tatu ambazo nitaiweka baadaye.