Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Buganda - Wikipedia

Buganda

From Wikipedia

Bendera ya Buganda
Bendera ya Buganda
Eneo la Buganda kati ya ziwa Viktoria, mto Nile na ziwa Kyoga
Eneo la Buganda kati ya ziwa Viktoria, mto Nile na ziwa Kyoga

Buganda ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Mfalme wa Buganda anatumia cheo cha Kabaka. Tangu karne ya 18 BK hadi karne ya 20 Buganda ilikuwa dola lenye enzi katika eneo la Ziwa Viktoria. Leo hii ni sehemu ya Uganda yenye madaraka ya kiutamaduni pamoja na kuwa na bunge lake la lakini si kitengo cha kiutawala ndani ya Uganda. Jina la nchi Uganda ni umbo la Kiswahili la neno Buganda.

[edit] Eneo na watu

Eneo la Buganda liko kaskazini na magharibi ya Ziwa Viktoria hadi mto Nile upande wa mashariki na ziwa Kyoga kaskazini. Watu wake huitwa Waganda (Kiganda: "Baganda") wanotumia lugha ya Kibantu kuna takriban milioni tatu ambao ni kabila kubwa la Uganda lenye 16.7% ya wakazi wote wa nchi. Kuna koo 52 kati ya Waganda.

Makaburi ya kihistoria ya wafalme wa Buganda huko Kasubi (Kampala) imeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.

[edit] Historia

Mwisho wa karne ya 19 Buganda ilikuwa lengo la majaribio ya nchi mbalimbali ya nje ambazo zilitaka kuwa na athari hapa. Wamisionari Wakatoliki kutoka Ufaransa na Waanglikana kutoka Uingereza walishindana na Waislamu kwenye ikulu ya Kabaka Mutesa I (1856–84) kati yao na dhidi ya wafuasi wa dini za jadi. Mashindano haya yalisababisha kutokea kwa vyama mbalimbali vilivyoleta nchi katika hali ya vurugo. Mnamo 1890 Mjerumani Karl Peters alifaulu kupata mkataba wa ushirikiano na Kabaka lakini serikali za Ujerumani na Uingereza zilipatana katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar nchi iwe eneo la athari ya Uingereza. Mwakilishi Mwingereza Frederick Lugard aliingilia kijeshi kati ya mapigano ya vikundi ndani ya Buganda na kuhakikisha utawala wa Kabaka Mwanga aliyehesabiwa kuwa upande wa Waanglikana hivyo karibu na Uingereza. Mwaka 1894 Kabaka alikubali mkataba wa ushirikiano na Uingereza ambao machoni pake ilikuwa mapatano ya hiari lakini hali halisi Buganda ikawa nchi ya kulindwa chini Uingereza.

Polepole utawala wa Kiingereza ilibadilisha hali ya Buganda hadi kuwa sehemu tu ya Uganda yote. Wakati wa uhuru Waganda walishindwa kupata hali ya ufalme kuwa sehemu ya nchi inayojitawala lakini Kabaka Sir Edward Mutesa II alikuwa Rais wa Taifa pamoja na waziri mkuu Milton Obote. Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini. Kwa muda wa miaka 30 ufalme wa Buganda ilifutwa kisheria. Kabaka Edward Mutesa II alikufa ng'ambo Uingereza.

Mwaka 1986 serikali mpya ya Yoweri Museveni ilimkaribisha mtoto wa Kabaka marehemu Ronald Muwenda Mutebi arudi Kampala. Baada ya Bunge la Uganda kurudisha falme za kihistoria ndani ya Uganda za Banyoro, Ankole na Toro pamoja na Buganda Mutebi alifanywa Kabaka mpya mwaka 1993.


[edit] External links

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com