Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Prussia - Wikipedia

Prussia

From Wikipedia

Prussia ni jina muhimu katika historia ya Ujerumani pia ya Poland.

Contents

[edit] Nchi ya Waprussia

Kisasili lamaanisha nchi ya Waprussia waliokuwa kabila ya Kibalti kaskazini-mashariki ya Poland kwenye pwani za bahari ya Baltiki. Mnamo mwaka 1200 BK Waprussia walikuwa katika hali ya vita na Poland. Mwaka 1226 mtawala wa Poland aliomba usaidizi wa jeshi wa wamisalaba Wajerumani akiwaahidi mali katika maeneo watakaoteka baada ya kushinda Waprussia.

[edit] Dola la Wamisalaba Wajerumani

Wamisalaba walifaulu kutekea eneo lilioitwa baadaya "Prussia ya mashariki" na kujenga himaya yao. Wamisalaba hawakuwa watemi wa kawaida bali wamonaki na wanajeshi. Dola la wamisalaba lilikuwa wakati mwingine chini ya mfalme wa Polandf, wakati mwingine dola la kujitegemea. Waliita walowezi na wakulima kutoka pande zote za Ujerumani na kuanzisha miji mingi.

Brandenburg na Prussia kati ya 1600 na 1800  biluu nyeusi: Brandenburg asilia; Kijani nyeusi: nyongeza 1618 ya Prussia; kijani: nyongeza nyingine 1600 hadi 1772; njano: nyongeza kutokana na ugawaji wa Poland
Brandenburg na Prussia kati ya 1600 na 1800
biluu nyeusi: Brandenburg asilia; Kijani nyeusi: nyongeza 1618 ya Prussia; kijani: nyongeza nyingine 1600 hadi 1772; njano: nyongeza kutokana na ugawaji wa Poland

[edit] Kuunganishwa na Brandenburg

Baada ya farakano kati ya Wakatoliki na Waprotestant himaya ya wamisalaba ilipokea uprotestanti na wamisalaba waliondoka katika maisha ya umonaki. Mkuu alikuwa mtemi mtawala akaoa.

Mkuu wa mwisho wa wamisalaba alikuwa mwana wa familia ya watemi wa Brandenburg katika Ujerumani hivyo Prussia imekuwa sehemu ya urithi wa familia hii iliyoendelea kutawala Prussia pamoja na maeneo yake ndani ya Ujerumani.

[edit] Ufalme wa Prussia

1701 mtemi Friedrich wa Brandenburg alijiwekea taji ya Mfalme wa Prussia.

Friedrich II wa Prussia
Friedrich II wa Prussia

Ufalme wa Prussia uliendelea kuwa muhimu kati ya madola ya Ujerumani. Watemi wa Brandenburg walirithi au kupata maeneo kwa njia ya vita hata katika magharibi ya Ujerumani. Mfalme Friedrich II wa Prussia alishindana na mataifa makubwa ya Ulaya katika vita ya miaka saba (1756-1763). Alikamata maeneo makubwa katika ugawaji wa Poland.

Prussia ilitokea kama dola la pili katika Dola takatifu la Ujerumani baada ya Austria.

Baada ya vita za Napoleoni mwanzo wa karne ya 19 umuhimu wa Prussia uliendelea kukua.

[edit] Prussia kama kiongozi wa Ujerumani

Katika ya vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Ujerumani 1866 Prussia ilishinda Austria na kuwa dola kiongozi kati ya madola ya Ujerumani. Mwanasiasa mkuu wa nyakati zile alikuwa Otto von Bismarck kama waziri mkuu wa Prussia na baadaye kama chansella wa Ujerumani. Baada ya kushinda Ufaransa katika vita ya 1871 sehemu zote za Ujerumani isipokuwa Austria ziliunganika chini ya uongozi wa Prussia na kuanzisha Dola la Ujerumani. Mfalme Wilhelm I wa Prussia alichaguliwa kuwa Kaisari wa Ujerumani. Alifuatwa na mtoto wake Friedrich III aliyekufa mapema halafu na Wilhelm II. Wakuu wale walitawala kwa cheo cha "Kaisari ya Ujerumani na mfalme wa Prussia".

Prussia (buluu nyeupe) ndani ya Ujerumani baada ya 1918
Prussia (buluu nyeupe) ndani ya Ujerumani baada ya 1918

[edit] Jamhuri ya Prussia ndani ya Ujerumani

Mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ufalme wa Prussia kama vile katika sehemu zote za Ujerumani ilifutwa katika mapinduzi ya Ujerumani ya 1918. Wilhelm II akajiuzulu na kukimbilia Uholanzi. Prussia ilikuwa jimbo jamhuri ndani ya jamhuri la shirikisho la Dola ya Ujerumani.

Baada ya Adolf Hitler kuchukua utawala wa Ujerumani na kujenga udikteta madaraka ya majimbo yote pia ya Prussia yalifutwa.

[edit] Mwisho wa Prussia

Mwaka 1945 mataifa washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia waliamua kutangaza mwisho wa Prussia wakiishtaki kuwa sababu ya tabia ya kivita ya Ujerumani. Maeneo ya Prussia yalifanywa kuwa majimbo katika Ujerumani kwa jumla. Prussia asilia yenyewe iligawiwa kati ya Poland na Urusi, wakazi wake Wajerumani walifukuzwa.

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com