Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Charles Darwin - Wikipedia

Charles Darwin

From Wikipedia

Charles Darwin kijana
Charles Darwin kijana

Charles Robert Darwin (12 Februari 1809 - 19 Aprili 1882) alikuwa mwanasayansi Mwingereza katika karne ya 19.

Amekuwa mshuhuri kutokana na nadharia yake ya mageuko ya spishi.

Nadharia hii yasema kuwa spishi zote za viumbehai vimetokana kutoka kwa spishi asilia zilizogeuka baada ya muda. Mageuko haya hufuata uteuzi asilia yaani viumbehai wanaolingana vizuri zaidi katika mazingira wanaishi na kuzaa kushinda viumbehai wasiolingana hivyo. Kwa njia hii tabia za viumbehai wanaofaa vizuri zaidi zinazidi kuendelezwa kwa sababu watoto wao hurithi tabia hizi. Lakini tabia za viumbehai wasiofaa sana zinaweza kupotea kwa sababu kwa sababu wanakufa mapema na hawana watoto wengi wanaoendeleza tabia zao.

[edit] Utoto na masomo

Alizaliwa mjini Shrewsbury (Uingereza) kama mtoto wa tano wa daktari Robert Darwin na Susannah Darwin (née Wedgwood). Baada ya kumaliza shule alijiunga na chuo kikuu cha Edinburgh (Uskoti) 1825 akajiandikisha katika idara ya tiba lakini hakupenda upasuaji. Alitumia muda mwngi kufuata kozi za biolojia, jiografia na jiolojia nje ya masomo ya tiba. Alifuatana mara nyingi na wataalamu walipofanya uchunguzi wa wanyama, mimea au mawe.

Baba baada ya kuona hafai kuwa daktari alimwandikisha katika masomo ya theolojia kwa shabaha ya kuwa mchungaji wa kanisa la kianglikana aliyomaliza mwaka 1831.

[edit] Safari ya MS Beagle

Safari ya Darwin kwenye Beagle
Safari ya Darwin kwenye Beagle

Baada ya kumaliza masomo haya Darwin alipata nafasi ya kujiunga kama mshiriki na safari ya kisayansi ya jahazi MS Beagle iliyotakiwa kuzunguka dunia yote kwa kusudi la kuboresha ramani hasa za pwani la Amerika Kusini. Darwin alipewa nafasi ya mwanaviumbe bila malipo ya kuongozana na kushauriana na nahodha na kiongozi wa safari kuhusu wanyama na mimea visivyojulikana na vitakavyopatikana safarini.

Katika safri hii Darwin aliona Amerika Kusini na visiwa vya Pasifiki. Akaona mengi na kushika kumbukumbu yake akakusanya mimea na miili ya wanyama na kuibeba naye kwa ajili ya maonyesho katika jumba la makumbusha la historia ya viumbe.

Kwenye visiwa vya Galapagos aliona ya kwamba kila kisiwa kilikuwa na spishi za ndege pia kobe zilivyotofautiana kidogo kati ya kisiwa na kisiwa.

Nakala ya 1859 ya kitabu Origins of Species
Nakala ya 1859 ya kitabu Origins of Species

[edit] Mapinduzi ya kisayansi

Baada ya kurudi Uingereza mwaka 1836 Darwin alianza kuchunguza sampuli zote alizokusanya. Alipata kazi kama katibu wa shirika la jiolojia.

Alipochungulia sampuli za Galapagos hasa alipata dhana ya kwamba spishi hizi zote za karibu zilitokana na aina moja tu iliyowahi kufika kwenye visiwa hivi lakini baadaye zilianza kuwa tofauti katika kila kisiwa na kuwa spishi ya pekee. Kama hii ilikuwa kweli spishi hizi hazikuumbwa hivyo tangu mwanzo.

Darwin aliendelea na utafiti wa sampuli zake na kutoa masomo mbalimbali na kuyatafakari. 1859 alitoa kitabu kuhusu ya mageuko ya spishi kwa njia ya uteuzi asilia (On the Origin of Species by Means of Natural Selection, or the Preservation of Favoured Races in the Struggle for Life) alimoeleza nadharia yake.

Kitabu kilikuwa kama bomu kati ya watu wa sayansi pia watu wa dini. Darwin alishambuliwa mara nyingi ya kuwa mafundisho yake yanapinga Biblia na taarifa ya uumbaji.

Leo hii nadharia yake inakubaliwa na wanasayansi karibu wote hata kama kuna kiasi cha upingamizi dhidi yake kwa sababu za kisayansi na kidini.

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com