Isaac Newton
From Wikipedia
Isaac Newton (4 Januari, 1642 – 31 Machi, 1727) ni mwingereza mwanamahesabu na fizikia anakumbukwa kama mwanasayansi maarufu duniani kutokana na michango yake mbali mbali katika sayansi. Ndiye aliyegundua tawi la calculus na nadharia ya mwendo. Newton alipata shahada yake ya kwanza mwaka 1665 na ile ya uzamili mwaka 1668. Mchango mwingine wa Isaac Newton upo katika nadharia ya mwanga, kuona na jinsi rangi zinavyotokea. Nadharia zake zote aliziweka katika vitendo na kukubalika na ndizo zitumumikazo leo.