Bahari ya Kaskazini
From Wikipedia
Bahari ya Kaskazini ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya Skandinavia (Norway na Denmark) upande wa mashariki, Ujerumani na Uholanzi upande wa kusini na Britania kwa magharibi.
Mlango wa bahari ya Skagerak unaiunganisha na bahari ya Baltiki. Mfereji wa Kiel inafupisha njia hii ukikata jimbo la Schleswig-Holstein ya Ujerumani. Kusini-magharibi kuna mlango wa Mfereji wa Kiingereza kati ya Britania na Ufaransa.
Kimo cha wastani ni 94 m pekee.
Mito mikubwa inayoingia katika Bahari ya Kaskazini ni pamoja na Rhine, Elbe, Weser, Ems, Meuse, Schelde, Thames na Humber.
Mabandari makubwa ni Rotterdam, Hamburg, Bremen na Antwerpen. Bahari ya Kaskazini ni kati ya bahari zinazopitiwa na meli nyingi duniani; zaidi ya robo ya usafiri wote wa baharini wa dunia unatokea hapo.
Katika sehemu za kaskazini kuna gesi na mafuta.