Duma
From Wikipedia
Duma ni mnyama katika kundi la wanyama walao nyama, yuko katika jamii ya paka. Ngozi yake ni manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi. Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Wanapokua, madume hutembea peke yao katika kundi duma watatu au wawili. Wanaungana na majike wanapokuwa kwenye joto tu na sivinginevyo. Rangi ya duma inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia katika mawindo yao. Ndiye mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao kwa miguu hukimbia kilometa 113 kwa saa. Chakula chake ni wanyama jamii ya swala hupatika Afrika na kidogo sehemu za Asia.