Antoine Henri Becquerel
From Wikipedia
Antoine Henri Becquerel (15 Desemba, 1852 – 25 Agosti, 1908) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ufaransa. Mwaka wa 1896 aligundua mionzi nururishi. Mwaka wa 1903, pamoja na Pierre na Marie Curie alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.