Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
William Booth - Wikipedia

William Booth

From Wikipedia

William Booth (10 Aprili 1829 – 20 Agosti 1912) alianzisha Jeshi la Wokovu na kuwa mkurugenzi wake wa kwanza (1878 – 1912).

William Booth
William Booth

Contents

[edit] Wasifu ya Maisha

[edit] Utoto na Ujana

Booth alizaliwa kijiji cha Sneiton, Wilaya ya Nottingham, nchi ya Uingereza. Alikuwa mmoja wa watoto wanne, lakini mwana wa kiume wa pekee wa Samuel Booth na Mary Moss. Baba yake alikuwa tajiri, lakini wakati wa utoto wake William Booth, familia walianza kuwa maskini.

Mwaka wa 1842, Samuel Booth ambaye wakati huo alikuwa amefilisika hakuweza kulipa ada za shule kwa William aliyekuwa na umri wa miaka 13. Hivyo William alianza kuwa mwanagenzi wa mweka rahani. Kabla mwaka huo haujaisha, baba yake alifariki.

Wakati wa uanagenzi wake William Booth aliingia Ukristo. Alianza kusoma vingi, kujifundisha kuandika na kutoa hotuba, na kuwa mhubiri mlei wa Kanisa la Metodisti. Alipomaliza uanagenzi wake mwaka wa 1848, alijaribu kupata kazi nyingine kwa vile hakupenda kazi ya mweka rahani. Mwaka wa 1849 alihama kutoka familia yake na kuhamia jiji la London ambapo alipata kazi katika duka la mweka rahani tena. Pia aliendelea na huduma ya mhubiri mlei lakini hakuridhika na nafasi alizozipata. Kwa hiyo aliacha kazi ya mhubiri mlei na kuanza huduma ya uinjilisti mitaani.

Mwaka wa 1851, Booth alijiunga na Kanisa la Wesley, na tarehe 10 Aprili 1852, yaani sikukuu yake ya kuzaliwa ya 23, aliacha kazi ya mweka rahani na kuwa mhubiri kwenye makao makuu yao kule Clapham. Baada ya wiki tano tu, alimchumbia Catherine Mumford. Mwezi wa Novemba 1852, Booth alialikwa kuwa mchungaji wa kanisa kule Spalding, Wilaya ya Lincolnshire.

[edit] Ndoa na watoto

William Booth na Catherine Mumford walifunga ndoa tarehe 16 Juni, 1855 katika kanisa la Stockwell Green kule London. Walikuwa na watoto wanane wafuatao:

  • Bramwell Booth (8 Machi 1856 – 16 Juni 1929).
  • Ballington Booth (28 Julai 1857 – 15 Octoba 1940).
  • Kate Booth (18 Septemba 1858 – 9 May 1955).
  • Emma Booth (8 Januari 1860 – 28 Octoba 1903).
  • Herbert Booth (26 August 1862 – 25 Septemba 1926).
  • Marie Booth (4 Mei 1864 – 5 Januari 1937).
  • Evangeline Booth (25 December 1865 – 17 Julai 1950).
  • Lucy Booth (28 Aprili 1868 – 18 Julai 1953).

[edit] Huduma yake ya kwanza

Ingawa Booth alikuwa mwinjilisti hodari, hakufurahia uchungaji. Mkutano wa kila mwaka wa kanisa lake walipoendelea kumpa majukumu ya uchungaji na kumkatalia ombi lake la kufanya uinjilisti tu, alijiuzulu uchungaji wake mwaka wa 1861.

Kwa vile dhehebu lake hawakumruhusu kufanya uinjilisti ndani ya makanisa baada ya kujiuzulu kwake, alikuwa mwinjilisti aliyejitegemea. Hata hivyo, teolojia yake haikubadilika. Aliendelea kuhubiri kwamba wasiookoka watateswa milele, kwamba kila mtu anahitaji kutubu, na kwamba Mungu anatuwezesha kuwa watakatifu, yaani tukiishi maisha ya upendo kwa Mungu na wenzetu. Hatimaye, hata watoto wa Booth walishirikisha katika huduma yake.

[edit] Misheni ya Kikristo (‘’The Christian Mission’’)

Mwaka wa 1865, Booth pamoja na mke wake walianzisha Shirika la Uamshaji la Kikristo (‘’Christian Revival Society’’)) katika eneo la East End la London. Waliendesha mikutano kila jioni na siku nzima ya Jumapili wakitoa huduma za toba, wokovu na maadili ya kikristo kwa fukara, pamoja na walevi, wahalifu na malaya. Jina la shirika lilibadilishwa baadaye kuwa Misheni ya Kikristo (‘’Christian Mission’’).

Booth na wanashirika wake walitenda walichohubiri, yaani waliishi maisha ya kikristo wakijitolea mhanga katika huduma kwa wengine. Kwa mfano, waligawa chakula kwa maskini bila kujali wakidharauliwa kwa ajili ya huduma zao za kikristo.

[edit] Jeshi la Wokovu

Mwaka wa 1878, jina la shirika lilibadilishwa tena kuwa Jeshi la Wokovu. Kama majeshi mengine, lilipata bendera yake na nyimbo zake ambazo hufuata sauti za watu wa kawaida zikiunganishwa na maneno ya kikristo. Booth na wanajeshi wengine huvaa sare za jeshi la Mungu kwenye mikutano. Booth alianza kuitwa Jenerali, na watumishi wengine walipewa vyeo vya afisa vilivyofaa.

Ingawa walibanwa kifedha, Jeshi la Wokovu na huduma zake zilienea haraka na kuzalia matawi katika nchi nyingine, baadhi yao Marekani, Ufaransa, Uswisi, Sweden, Australia, Kanada, Uhindi, Afrika ya Kusini, New Zealand, Jamaika, na kadhalika.

Wakati wa maisha yake, William Booth alianzisha huduma za Jeshi la Wokovu katika nchi 58 akisafiri sana na kuendesha mikutano. Booth alitoa jarida na kuandika vitabu kadhaa. Pia alitunga nyimbo nyingi. Kitabu chake maarufu kabisa ni In Darkest England and the Way Out kilichotolewa mwaka wa 1890.

[edit] Miaka ya mwisho

Hatimaye huduma za Jeshi la Wokovu na za William Booth ziliheshimiwa hadharani. Mwishoni mwa maisha yake, Booth alipokelewa na wafalme na maraisi. Hata vyombo vya habari walimwita Jenerali kwa kumheshimu.

William Booth aliaga dunia wakati alipokuwa amefikisha umri wa miaka 83. Alizikwa kwenye Abney Park Cemetery ambapo na mke wake alikuwa amezikwa. Ili kumheshimu Booth, mshairi Vachel Lindsay aliandika shairi liitwalo General William Booth Enters Into Heaven, na Charles Ives aliyekuwa jirani wa Booth alitunga sauti kwa shairi hilo.

[edit] Marejeo ya nje

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com