Dogali
From Wikipedia
Dogali katika tambarare ya pwani la Eritrea takriban 30 km kutoka Massawa ni mahali pa mapigano kati ya kikosi cha Waitalia na jeshi la Waethiopia tarehe 24 Januari 1887.
Kikosi cha Waitalia 587 walielekea kaskazini kutoka Massawa kilishambuliwa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus wa Ethiopia. Karibu Waitalia 500 waliuawa ni 80 wajeruhiwa pekee walioweza kurudi.
Kuna obeliski huko Roma na makaburi ya kiitalia kwenye mahali penyewe ya kukumbuka Waitalia waliokufa.