Web - Amazon

We provide Linux to the World


We support WINRAR [What is this] - [Download .exe file(s) for Windows]

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
SITEMAP
Audiobooks by Valerio Di Stefano: Single Download - Complete Download [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Alphabetical Download  [TAR] [WIM] [ZIP] [RAR] - Download Instructions

Make a donation: IBAN: IT36M0708677020000000008016 - BIC/SWIFT:  ICRAITRRU60 - VALERIO DI STEFANO or
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Baada ya Kristo - Wikipedia

Baada ya Kristo

From Wikipedia

Baada ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka. Hesabu hii imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani siku hizi. Kila mwaka huhesabiwa kuanzia mwaka unaodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

Contents

[edit] Historia ya Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo"

Hesabu hii ilianzishwa mnamo mwaka 532 BK na mmonaki Mroma Dionysius Exiguus. Wakati wake mahesabu mbalimbali yalikuwa kawaida. Mwaka uleule uliweza kuitwa kutokana na muda wa utawala wa Mfalme au Kaisari (kwa mfano: mwaka wa tano wa Kaisari Iustiniano)na pia kuanzia tarehe ya kuundwa kwa mji wa Roma (kwa mfano: mwaka 1185 ab urbe condita = tangu kuanzishwa kwa mji). Mahesabu mengine yaliyokuwa kawaida wakati uleule ni makadirio mbalimbali "tangu kuumbwa kwa dunia" na mengine. Dionysio baada ya kufanya utafiti aliona Yesu alizaliwa mwaka 754 tangu kuanzishwa kwa Roma.

Hesabu hii haijui mwaka "0"; tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu huchukuliwa kama mwanzo wa mwaka. Kwa hiyo moja kwa moja inainhgia katika mwaka "1"- na mwaka kabla yake ni mwaka 1 kabla ya Kristo = KK.

Hii ni sababu ya kwamba dunia karibu lote lilikosa kusheherekea mwaka 2000 kuwa mwanzo wa milenia mpya. Mwaka 2000 ilikuwa mwaka wa mwisho wa karne iliyoanza mw. 1901; karne na milenia mpya ilianza mwaka 2001.

[edit] Kosa la Hesabu ya Dionysio

Hesabu ya Dionysio ilikuwa na kosa ya miaka kadhaa. Wakati wake Dola la Roma lilikuwa limeshakwisha katika Italia, Kaisari alikaa Bizanti au Roma ya Mashariki. Kumbukumbu za Roma yenyewe hazikutunzwa tena tangu miaka mingi. Leo hii wataalamu wengi hukubaliana ya kwamba kasoro la Dionysio ni takriban miaka 4 - 8; yaani mwaka halali wa kuzaliwa kwake Yesu ulikuwa kama miaka nne hadi nane kabla ya mwaka ambao tumezoea kuhesabu kama "1". Wengi walijaribu kusahihisha kosa hili lakini habari kamili kabisa hazipatikani tena.

[edit] Uenezaji wa Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo"

Mwanzoni hesabu ya Dionysio ilikuwa pendekezo la mtaalamu fulani tu watu wakiendelea kutumia mahesabu yao mbalimbali. Miaka 60 baada ya Dionysio mkuu wa kanisa katoliki Papa Bonifatio IV anajulikana alitumia tarehe zote mbili za "baada ya Kristo" na "tangu kuanzishwa kwa mji". Wataaaaalamu walianza kutumia zaidi hesabu hiyo. Wakati wa Mfalme (baadaye alichukua cheo cha Kaisari) Karolo Mkuu aliyetawala Ufaransa pamoja na Ujerumani, Italia ya Kaskazini na maeneo ya Uholanzi na Ubelgiji ya kwamba hesabu tangu Kristo ilikuwa hesabu rasmi ya serikali. Lakini bado ilihitajika karne kadhaa hadi hesabu hii imekuwa kawaida katika Ulaya.

Kutokana na uenezaji wa uchumi, biashara na utawala wa Kiulaya duniani hesabu "Baada ya Kristo" ilienea kote duniani. Siku hizi ni hesabu ya pekee katika nchi nyingi. Katika nchi mbalimbali inatumika sambamba na mahesabu mengine. Nchi za Kiislamu mbalimbali hutumia miaka tangu Hijra ya Mtume Mohammed (mw. 622 BK), lakini mara nyingi pamoja na miaka ya hesabu ya kikristo kwa ajili ya mambo ya biashara na mawasiliano ya kimataifa.

Nchi ya Israel inatumia kalenda rasmi tangu "kuumbwa kwa dunia", isipokuwa vilevile kandokando na Kalenda ya BK kwa sababu zilizotajwa hapa juu kwa ajili ya nchi za Kiislamu.

Japan inatumia hesabu ya miaka ya Kaisari yake - vilevile kandokando na Kalenda ya BK.

[edit] Namna za kutaja Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo"

Dionysio hakutumia lugha "baada ya Kristo" - alisema "Anno Domini natum" ("mwaka tangu kuzaliwa kwake Bwana") akimaanisha Dominus = Bwana ndiye Yesu. Hivyo kifupi katika lugha ya Kilatini ni "AD" kilichoingia pia katika Kiingereza. AD hivyo inamaanisha kwa kifupi "Anno Domini" au "Mwaka wa Bwana".

Hata miaka kabla ya Kristo kwa Kiingereza huitwa kwa kifupi cha Kilatini "a. Chr" (ante Christum natum = kabla ya kuzaliwa kwake Kristo). Wengine hutumia "BC" = "before Christ".

Our "Network":

Project Gutenberg
https://gutenberg.classicistranieri.com

Encyclopaedia Britannica 1911
https://encyclopaediabritannica.classicistranieri.com

Librivox Audiobooks
https://librivox.classicistranieri.com

Linux Distributions
https://old.classicistranieri.com

Magnatune (MP3 Music)
https://magnatune.classicistranieri.com

Static Wikipedia (June 2008)
https://wikipedia.classicistranieri.com

Static Wikipedia (March 2008)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com/mar2008/

Static Wikipedia (2007)
https://wikipedia2007.classicistranieri.com

Static Wikipedia (2006)
https://wikipedia2006.classicistranieri.com

Liber Liber
https://liberliber.classicistranieri.com

ZIM Files for Kiwix
https://zim.classicistranieri.com


Other Websites:

Bach - Goldberg Variations
https://www.goldbergvariations.org

Lazarillo de Tormes
https://www.lazarillodetormes.org

Madame Bovary
https://www.madamebovary.org

Il Fu Mattia Pascal
https://www.mattiapascal.it

The Voice in the Desert
https://www.thevoiceinthedesert.org

Confessione d'un amore fascista
https://www.amorefascista.it

Malinverno
https://www.malinverno.org

Debito formativo
https://www.debitoformativo.it

Adina Spire
https://www.adinaspire.com