Maria Goeppert-Mayer
From Wikipedia
Maria Goeppert Mayer (28 Juni, 1906 – 20 Februari, 1972) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa Ujerumani na kuhamia Marekani mwaka wa 1930 baada ya kuolewa na Mmarekani Joseph Mayer. Hasa alichunguza nadharia ya atomu. Mwaka wa 1963, pamoja na J. Hans D. Jensen na Eugene Wigner alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.