Elizabeth Ann Seton
From Wikipedia
Elizabeth Ann Seton (28 Agosti, 1774 – 4 Januari, 1821) alikuwa mwanzishi wa jumuiya ya Masista wa Huruma (kwa Kiingereza Sisters of Charity), jumuiya ya kikatoliki ya kwanza huko Marekani. Hasa alifundisha na kuwasaidia watoto maskini wengi. Mwaka wa 1975 alitangazwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 4 Januari.