Venezuela
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: None 2 | |||||
Wimbo wa taifa: Gloria al Bravo Pueblo | |||||
Mji mkuu | Caracas |
||||
Mji mkubwa nchini | Caracas | ||||
Lugha rasmi | Kihispania 3 | ||||
Serikali
Rais
|
Shirikisho la jamhuri Hugo Chávez Frías |
||||
Uhuru Kutoka Hispania Kutoka Gran Colombia ilitambuliwa |
5 Julai 1811 21 Novemba 1831 30 Machi 1845 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
916,445 km² (ya 33) 0.3 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
26,749,000 (ya 43) 23,054,210 29/km² (ya 175) |
||||
Fedha | Bolivar (VEB ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) None (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .ve | ||||
Kodi ya simu | +58 |
||||
1 Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela imekuwa jina la nchi tangu katiba ya 1999. "Kibolivar" ni jina la heshima kwa kumbukumbu ya mshujaa wa uhuru Simon Bolivar. 2 Zamani: Dios y Federación ("Mungu na Shirikisho") 3 Katiba inatambua pia lugha asilia zote nchini. |
Venezuela ni nchi katika Kaskazini ya Amerika ya Kusini. Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.
Mbele ya pwani la nchi katika Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.
Venezuelea ilikuwa koloni ya Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.
Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri na mji mkuu wa kitaifa ni Caracas.
Contents |
[edit] Asili ya jina "Venezuela"
Jina la nchi ni umbo la Kihispania la jina la mji wa Venezia (Italia). Mpelelezi Mwitalia katika utumishi wa mfalme wa Hispania Amerigo Vespucci aliona vijiji vya wenyeji waliojenga nyumba juu ya maboriti yaliyosimamishwa katika maji karibu na mwambao pasipo na kina. Vijiji vilimkubusha juu ya mji wa Venezia uliojengwa vile. Venezuela yamaanisha "Venezia Ndogo" katika Kihispania.
[edit] Jiografia
Venezuela ina eneo la 916,445 km² (kama Namibia) ikiwa na pwani lenye urefu la 2,800 km. Asilimia 39 za eneo hili ni misitu, mashamba ya kulimwa 4%, eneo la mifugo 20%, mazao ya kudumu kama kahawa 1%.
Kuna kanda nne za kijiografia:
- tambarare za pwani karibu na Maracaibo katika kaskazini-magharibi
- milima ya Andes
- tambarere za mto Orinoko katikati ya nchi
- nyanda za juu za Guayana katika kusini-mashariki
[edit] Milima ya meza
Nyanda za juu za Guayana zina milima ya pekee kuna milima ya meza 115 inayoitwa "tepui" katika lugha ya wenyeji asilia. Kiekolojia hii ni eneo muhimu kwa sababu milima mingi ina mimea na wanyama za pekee tofauti na milima jirani inayopatikana hapa tu kote duniani.
Maporomoko marefu duniani yatelemka kutoka milima hii kama vile maporomoko Salto del Angel ("anguko la malaika") ambako maji huanguka mita 965.
[edit] Mito
Mto mkubwa wa Venezuela ni Orinoco mwenye urefu wa 2574 km unaoishia katika Atlantiki. Lakini mkono wa Brazo Casiquiare unajitenga na kuishia katika mto wa Amazonas nchini Brazil.
Tawimito muhimu ya Orinoco ni Rio Apure na Rio Caroni.
[edit] Majimbo katika shirikisho
Venezuela ni shirikisho la madola au majimbo 23 ya kujitawala, maeneo yasiyojitawala na mkoa wa shirikisho la Caracas.
Jimbo | Mji Mkuu | Wakazi | Eneo | Kanda | |
---|---|---|---|---|---|
Amazonas | Puerto Ayacucho | 70,464 | 180,144 km² | Guayana | |
Anzoátegui | Barcelona | 1,222,225 | 43,300 km² | Nor - Oriental | |
Apure | San Fernando de Apure | 377,756 | 76,500 km² | Llanos | |
Aragua | Maracay | 1,449,616 | 7,014 km² | Central | |
Barinas | Barinas | 624,508 | 35,200 km² | Andean | |
Bolívar | Ciudad Bolívar | 1,214,846 | 238.000 km² | Guayana | |
Carabobo | Valencia | 1,932,168 | 4,650 km² | Central | |
Cojedes | San Carlos | 253,105 | 14,800 km² | Central | |
Delta Amacuro | Tucupita | 97,987 | 40,200 km² | Guayana | |
Falcón | Coro | 763,180 | 24,800 km² | Central - Occidental | |
Guárico | San Juan de los Morros | 627,086 | 64,986 km² | Llanos | |
Lara | Barquisimeto | 1,556,415 | 19,800 km² | Central - Occidental | |
Mérida | Mérida | 715,268 | 11,300 km² | Andean | |
Miranda | Los Teques | 2,330,872 | 7,950 km² | Capital | |
Monagas | Maturín | 712,626 | 28,930 km² | Nor - Oriental | |
Nueva Esparta | La Asunción | 712,626 | 1,150 km² | Insular | |
Portuguesa | Guanare | 725,740 | 15,200 km² | Central - Occidental | |
Sucre | Cumaná | 786,483 | 11,800 km² | Nor - Oriental | |
Táchira | San Cristóbal | 992,669 | 11,100 km² | South - Occidental | |
Trujillo | Trujillo | 608,563 | 7,400 km² | Andean | |
Vargas | La Guaira | 298,109 | 1,496 km² | Capital | |
Yaracuy | San Felipe | 499,049 | 7,100 km² | Central - Occidental | |
Zulia | Maracaibo | 2,983,679 | 63,100 km² | Zulian | |
Dependencias Federales (maneo chini ya shirikisho) | - | 2,245 | 342 km² | Insular (visiwa) | |
Distrito Federal Caracas (Mkoa wa shirikisho) | - | 2,284,921 | 433 km² | Capital (mji mkuu) |