Help:Contents
From Wikipedia
Ukitaka kubadili, kusahihisha au kuhariri makala, ubonyeze "hariri" kule juu katika ukurasa wowote.
Ukitaka kuanzisha makala mpya, utengeneze kwanza kiungo kwa makala hiyo kutoka ukurasa mwingine kwa kutumia mabano mraba: [[ na ]]. Kwa mfano, ukitaka kuanzisha ukurasa kuhusu Kijerumani, andika [[Kijerumani]] katika makala ya lugha (katika sehemu ya "kurasa zinazohusiana"). Baadaye, ubonyeze kiungo hicho, na uandike makala.
Ukitaka kujua ufanye nini ili kusaidia kuboresha kamusi elezo hii, angalia Ukurasa wa jumuia.
[edit] Picha
Ukitaka kutumia picha iliyopo katika Wikipedia ya lugha nyingine, unatakiwa kwanza kuweka picha hiyo katika kompyuta yako. Baada ya hapo, unaweza kuiweka Wikipedia ya Kiswahili.
Kwa kuweza kuingiza picha katika Wikipedia ya Kiswahili, unatakiwa kuingia kwa kutumia jina lako (bofya juu kulia), halafu chini kushoto utapata kiungo kinachoitwa "Pakia faili" (chini ya andiko "vifaa"). Bofya kiungo hicho.
Katika ukarasa ujao, unabofya "Durchsuchen" na kuchagua faili ya picha katika kompyuta yako. Halafu bofya "Upload file", na picha itakuwemo Wikipedia ya Kiswahili.
Unaweza kutumia picha kwa kuandika [[Image:jina_la_picha.jpg]].
[edit] Kuelekeza
Mara nyingi inatokea kwamba majina mawili yanafaa kwa makala fulani. Ikiwa hivi, lazima tuamue makala ipatikane chini ya jina gani. Lakini tunaweza kuelekeza kutoka jina jingine kwa jina sahihi la makala, ili watu waipate makala rahisi zaidi.
Ili kuelekeza kutoka jina moja kwenda jina sahihi la makala, tumia
- #REDIRECT[[Jina la makala]]
Unaweza kuangalia mfano huu: Abunuwasi.