Zambezi (mto)
From Wikipedia
Mto wa Zambezi | |
---|---|
|
|
Chanzo | karibu na Mwinilunga, Zambia |
Mdomo | Bahari ya Hindi |
Nchi za beseni ya mto | Zambia, Kongo, Angola, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji |
Urefu | 2,574 km |
Kimo cha chanzo | 1,500 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 7,000 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 1,570,000 km² |
Zambezi ni kati ya mito mirefu ya Afrika ikiwa na nafasi ya nne baada ya Nile, Kongo na Niger. Ni mto mrefu wa Afrika wa kuingia Bahari Hindi. Beseni yake ina 1,570,000 km² au nusu ya mto Nile. Chanzo chake iko Zambia inapita Angola mpakani na Namibia, Botswana, Zambia na Zimbabwe kwenda Msumbiji inapofikia Bahari Hindi katika delta ya 880 km².
Kwenye mwendo wa Zambezi pana maporomoko kadhaa hasa maporomoko ya Victoria Falls. Mengine ni maporomoko ya Chavuma mpakani wa Zambia na Angola halafu Ngonye Falls karibu na Sioma, Zambia ya magharibi.
Zambezi ina madaraja matano pekee kati ya chanzo na mdomo mahali pafuatapo: Chinyingi, Katima Mulilo, Victoria Falls, Chirundu na Tete.
Zambezi ni chanzo cha umeme kwa ajili ya sehemu kubwa ya Afrika ya Kusini. Umeme unatengenezwa kwa nishati ya maji huko lambo la Kariba (Zambia) na lambo la Cabora-Bassa (Msumbiji).
[edit] Tawimito
Tawimito muhimu ni Cuando, Kafue, Luangwa, Shire.
[edit] Miji muhimu mtoni
- Mongu
- Lukulu
- Katima Mulilo (Namibia), Sesheke (Zambia)
- Livingstone (Zambia), Victoria Falls (Zimbabwe)
- Kariba
- Songo
- Tete