Tanganyika (ziwa)
From Wikipedia
Ziwa la Tanganyika | |
---|---|
|
|
Mahali | Afrika ya Mashariki |
Nchi zinazopakana | Burundi, Kongo, Tanzania, Zambia |
Eneo la maji | 32,893 km² kutegemeana na kiasi cha mvua |
Kina ya chini | kuanzia 3.5 m |
Mito inayoingia | Lufubu, Malagarasi, Ruzizi |
Mito inayotoka | Lukuga |
Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB | 782 m |
Miji mikubwa ufukoni | Bujumbura, Kalemie, Kigoma |
Ziwa la Tanganyika ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya kati ikiwa eneo lake ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika na ujazo wa maji yake ya pili duniani baadaya Ziwa Baikal. Ujazo wake mkubwa umetokana na vilindi vyake vinaelekea chini hadi mita 1470. Urefu wa ziwa ni 673 km na upana wake takriban 50 km. Eneo la maji ni 32,900 km².
Ziwa la Tanganyika limepakana na nchi zifuatazo: Kongo, Tanzania, Burundi na Zambia. Kongo na Tanzania zinatawala sehemu kubwa ya ziwa.
Beseni ya ziwa ni 231,000 km². Mito miwili mikubwa ya Ruzizi na Malagarasi inapeleka maji yao ziwani. Maji yanatoka kwa njia ya mto Lukuga kwenda mto Kongo.
Miji mikubwa ziwani ni mabandari ya Kigoma kwa upande wa Tanzania na Kalemie kwa upande wa Kongo. Kila bandari ni pamoja na mwanzo wa njia ya reli.