Jean-Paul Sartre
From Wikipedia
Jean-Paul Sartre (21 Juni, 1905 – 15 Aprili, 1980) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchi ya Ufaransa. Alikuwa mtetezi mkuu wa falsafa ya "Existentialism". Falsafa hiyo inakiri kwamba hakuna mantiki ambayo mtu angeweza kuitumia kwa ajili ya maamuzi yake, lakini lazima kila mtu afanye uchaguzi yeye mwenyewe na atawajibika kwa matendo yake. Mwaka wa 1964 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi lakini aliikataa.